Kituo cha Athari ya Ufadhili wa Kimasomo wa Majaribio

Pilot Scholarship Impact Hub Photo: Kituo cha Athari ya Ufadhili wa Kimasomo wa Majaribio

Kituo cha Athari ya Ufadhili wa Kimasomo wa Majaribio

Ufadhili wa kimasomo unaweza kuwa usaidizi mkubwa zaidi wa kukabili umasikini, kutoa mafanikio binafsi na maendeleo ya kijamii. Fedha nyingi zimewekezwa kusaidia ufadhili wa Kiafrika wa kimasomo na serikali, wakfu, kampuni, mashirika yasiyo ya serikali na watu binafsi.

Ufadhili wa kimasomo pia umetajwa kuwa sehemu muhimu katika kufanikisha Lengo la Maendeleo ya Mkakati (SDG 4) la Umoja wa Mataifa.

Ilhali inaweza kuwa vigumu kwa watoa ufadhili wa kimasomo kuwafikia wasomi wenye uwezo na walio na wasifu unaohitajika kwa njia ya gharama nafuu na hata vigumu zaidi kwa wasomi wenye uwezo wa kupata ufadhili mwafaka wa kimasomo. Wanafunzi wengi wanaostahiki wanajitahidi kuweka pamoja ufadhili mbalimbali wa kimasomo wa kufanya na kukamilisha kozi zao. Kukiwa na hitaji linaloongezeka la maeneo ya vyuo vikuu, mahangaiko haya yatazidi kuongezeka katika miaka ijayo. 

Ni haki, kutokana na mazingira mbalimbali ambayo hutumikia, kwamba kuna mifano mingi ya mipango ya ufadhili wa kimasomo. Hata hivyo, si yote ambayo ina msingi wa ushahidi au kuendeshwa na athari na kunaonekana kuna uonekanaji mchache kwenye Viashiria Vikuu vya Utendaji (KPIs) vinavyotumika kupima athari

Mara nyingi, fedha huwa zinatumika kimkakati badala ya kuwekezwa kimkakati. Kwa mfano, hakuna 'kujiunganisha' katika maeneo yenye uhaba wa ujuzi muhimu kutokana na mifumo michache sana ya ufanisi ya kushiriki mazoea bora au kuwaunganisha wadau.

Uzoefu wetu na wanafunzi, shule na vyuo vikuu katika nchi za barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara na watoaji ufadhili wa kimasomo unaonyesha kwamba kuna fursa ya Afrika 'kuzidi' mawazo na mazoea ya ulimwengu katika nyanja hii.

Kwa kujaribu 'Kituo cha Athari ya Ufadhili wa Kimasomo' jukumu la ESSA litasaidia kugeuza fursa hii kuwa kweli, na kuangazia kile tunachoamini kuwa suala kuu la kimkakati kwa sekta ya Elimu ya Juu pamoja na shule na wafadhili.

 

Malengo Yetu

  • Kuongeza athari kwenye matumizi ya sasa, kuvutia uwekezaji zaidi katika ufadhili wa kimasomo barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara na lengo kuu likiwa kuboresha matokeo ya kielimu 

  • Kuthibitisha mfumo na kutoa pendekezo la uwekezaji ili mfadhili mkuu atusaidia kupanua jaribio hii na kulidumisha.

 

Jaribio hili litazingatia dhana tatu zinazohusiana na Mafunzo ya Elimu ya Afrika Kusini mwa Afrika Kusini mwa Sahara:

Kusanya: "Thibitisha haja na fursa kwa ushahidi thabiti"

Kazi yetu itazingatia ufadhili wa kimasomo wa Shahada ya Kwanza na ya Uzamili/Uzamilifu.  

Tutatambua mipango yenye ufanisi zaidi, tuangalie mifano yake kwa undani na kutambua vipengele vyake muhimu vya mafanikio kuanzia uteuzi wa ufadhili wa kimasomo hadi uhitimu na hata zaidi. 

Tunataka kuzalisha ushahidi thabiti wa kutumia ili kuanza kutengeneza njia za vitendo za kusaidia kubadilisha.

Unda – "Rasilimali, Mahusiano na Uaminifu" 

Lengo letu ni ktengeneza rasilimali muhimu, kujenga mahusiano na jamii katika nyanja hii na kuanzisha uaminifu muhimu kuhamasisha na kuleta mabadiliko. 

Mfano mmoja wa hili utakuwa kuzalisha kundi la metriki za athari za ufadhili wa kimasomo ikiwa ni pamoja na mafanikio ya msomi, mfadhili na mwasilishaji na vilevile ufanisi na athari kwa jamii. Pia tutaonyesha mifano ya mazoea bora, mifano na mwenendo muhimu pamoja na mawazo mapya ya kufikiri. Mapema, tunalenga kuwapa wasomi "sauti" na kuwahusisha kikamilifu katika yote tunayofanya.  Pia tunaona kujenga jamii ya mashirika kama hatua nyingine muhimu. 

Tutaimarisha hili kwa rasilimali za vitendo, ikiwa ni pamoja na vifaa vya dijitali na rasilimali za mafunzo kwa wanafunzi, wafadhili na wawasilishaji katika hatua zote za mchakato – kuanzia kutuma maombi, masomo, hadi kutafuta kazi nzuri na pia kuanzisha/kusimamia mpango wa ufadhili wa kimasomo.

Kujenga ujuzi na uwezo wa kufanya hivyo na kutoa kwa viwango vidogo ni hatua muhimu katika kuunda Kituo endelevu cha Athari ya Ufadhili wa Kimasomo.

Kuwasilisha – "Anza kuhamasisha na kubadili majadiliano"

Mazungumzo ya mapema kuhusu dhana ya kujenga Kituo cha Athari ya Ufadhili wa Kimasomo kutoka kwa wadau mbalimbali yamekuwa ya kutia moyo sana.  

Wakati wa majaribio haya, tunataka kuanzisha mabadiliko na kuanza kubadilisha majadiliano kwa ushahidi wa mazoea bora na mifano bora zaidi ikichukua nafasi kuu katika kufanikisha hili. Kushirikisha makundi ya sasa yaliyogawanyika itakuwa nafasi nyingine. Tutazalisha njia mbalimbali za mawasiliano na fursa kwa wale walio katika nyaja hii ili kushirikiana katika masuala yote ya kimkakati na ya uendeshaji.

 

Mradi huu unaambatana kikamilifu na kusudi letu la "Kujiunga, kufahamisha. Kuhamasisha na kuongeza athari kwa kila mtu anayewekeza katika matokeo ya elimu barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara."

PARTNERS

The Schaufler Foundation
The Schaufler Foundation

The Schaufler Foundation was founded in 2005 by Senator h. c. Peter Schaufler (deceased), former CEO and owner of BITZER, with the aim to continue his life’s work of combining entrepreneurship with science, research, education and the arts.

In terms of science and research, the focus is on environment protection. In the field of education, the foundation supports a variety of universities in Germany and now, by working with ESSA, will expand its activities into Africa.  The Schaufler Foundation is a key funder of ESSA's Pilot Scholarship Impact Hub project.

The Schaufler Foundation also funds the Schauwerk Sindelfingen, a museum for contemporary art.  Since its opening in June 2010, the Schauwerk Sindelfingen has displayed a representative selection of over 3,500 works from the Schaufler collection, together with loans from other museums and collectors as part of its temporary exhibitions.

The Schaufler Foundation

 

Student Scholarship Survey

ESSA is conducting a survey of African students currently in receipt of a scholarship and also alumni who received a scholarship during the past five-seven years.  The survey takes no more than ten minutes to complete and will help us with our work on this project. 

Survey link