Rasilimali

Tunavyokua tutaongeza rasilimali mbalimbali kwenye tovuti yetu. Ya kwanza, 'Hifadhidata ya Kituo cha REAL na ESSA ya utafiti wa Kiafrika kuhusu elimu' itakuja hivi karibuni.

Hifadhidata ya utafiti

Inaweza kuwa vigumu kupata utafiti bora wa Kiafrika kuhusu mada ya elimu na hata vigumu zaidi kwa watafiti Waafrika kuchapisha kazi zao na kufanikisha ufahamu na ushawishi. Tunataka kubadilisha hili..

Pamoja na Kituo cha REAL katika Chuo Kikuu cha Cambridge, hatua ya kwanza imechukuliwa kwa kuleta ushahidi wenye msingi wa utafiti uliofanywa na watafiti walioko barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara. Kutokana na hii, hifadhidata wazi, tangamanifu na inayoweza kutafutika za utafiti wenye misingi wa Afrika kuhusu Elimu barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara imeundwa ambayo hivi karibuni itapatikana kwenye tovuti za ESSA na Kituo cha REAL. Blogi iliyo hapa chini inatoa maelezo zaidi kuhusu kinachofuata.    

 

"Kujifunza, ukikitumia, huongezeka": hifadhidata ya utafiti wa elimu ya Afrika ili kujuza kuhusu sera na utekelezaji na Rafael Mitchell na Pauline Rose

Soma makala

Wasilisha mapendekezo ya kuingizwa kwenye Database ya Utafiti wa Elimu ya Kiafrika.

Tuma mapendekezo

 

"Mapping the landscape of education research by scholars based in sub-Saharan Africa"

Download the report

openESSA

Kutokana na ushirikiano baina ya ESSA na  Taasisi ya Hasso Plattner , hii itajumuisha OpenESSA jukwaa jipya tangamanifu, la mtandaoni, na kuhamisha maarifa ambalo litakuwa na rasilimali mbalimbali za kidijital kutoka kwa wachangiaji wadogo hadi kwa miongozo, mazungumzo na mihadhara pamoja na MOOCS zilizoidhinishwa na rasilimali nyingine kuhusu mada za umuhimu.

 Pia itajumuisha kalenda ya kimataifa ya matukio yanayohusiana na elimu Afrika ya Jangwa la Sahara na baada ya muda itakuwa na mengi zaidi.

Kinachofuatia

Kutumia mbinu ya hatua kwa hatua, tutaongeza rasilimali muhimu zaidi kwenye tovuti yetu kwa wale wanaotaka kubadilisha matokeo ya kielimu Afrika ya Jangwa la Sahara. 

 

 

Ili kupata maelezo zaidi na muhtasari wa kazi yetu tafadhali pakua kipeperushi chetu.  

Pakua