Washirika

Kuanzia mwanzo ESSA imekuwa ikishirikiana na washirika wa ndani na nje ya Afrika ambao wanashiriki maono na imani yetu kwamba kwa kufanya kazi pamoja kila mmoja wetu atafanikiwa zaidi katika kufanikisha malengo yetu

Taasisi ya Africa America (AAI)
Taasisi ya Africa America (AAI)

Misheni ya AAI ni kuimarisha uwezo wa binadamu kwa ajili ya maendeleo ya Afrika kupitia elimu, mafunzo ya ujuzi, mazungumzo, shughuli za kongamano, utengenezaji na usimamiaji mipango. AAI ina jukumu muhimu katika kufanikisha ushirikiano kati ya Marekani na Afrika.

 AAI imeipa ESSA jukwaa la uwasilishaji wa kwanza wa umma wa kazi yake mwaka 2017 kwenye mkutano wao wa SOE mjini Nairobi . Hivi sasa tunafanya kazi pamoja ili kuendeleza mradi kuhusu "Data na takwimu za Hali ya Kielimu barani Afrika"

"ESSA ni jitihada mpya ya kuvutia katika nyanja ya elimu ya Kiafrika – ninafurahia sana ubunifu wa ESSA na hatua yake na mkabala wake wa athari katika kukabiliana na changamoto kubwa."

Kofi Appenteng, Afisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Africa-America, New York City

The Africa-America Institute (AAI)

Chama cha Vyuo Vikuu Afrika (AAU)
Chama cha Vyuo Vikuu Afrika (AAU)

AAU ni mmoja wa washirika muhimu katika elimu ya juu barani Afrika. Ikiwa na zaidi ya wanachama 400, misheni yake ni kuongeza ubora na umuhimu wa elimu ya juu barani Afrika na kuimarisha mchango wake katika maendeleo ya Afrika.

Kutoka makao yake makuu nchini Ghana, AAU inahudumu kama jukwaa la Vyuo Vikuu vya Afrika kushirikiana katika utafiti na kutafakari na kushauriana juu ya masuala ya Elimu ya Juu. Ina uwezo wa kipekee wa kuungana na kuwasiliana na viongozi wa taasisi na watunga sera kutoka sehemu zote za Afrika. 

AAU iliunda ushirikiano na ESSA mwaka 2017 na tumekuwa tukifanya kazi pamoja katika miradi mbalimbali, hasa "Demografia za Kitivo" na kuundwa kwa "Bodi ya Kazi za Usomi ya Pan-Afrika".  AAU pia iliipa ESSA jukumu kubwa katika kongamano lake la 2017 la Maadhimisho ya Miaka 50 mjini Accra, katika kupanua mtandao wa ESSA na sifa katika hatua ya mwanzo katika maendeleo yake.

"ESSA ni mshirika mkuu kwa AAU na ninafurahia sana mawazo yao safi, mkabala thabiti na njia yao ya ushirikiano ya kufanya kazi. 'Kuunganisha' ni sehemu ya DNA yao!"

Prof. Etienne Ahile, Katibu Mkuu, Chama cha Vyuo vikuu vya Afrika

 

Chama cha Vyuo Vikuu Afrika (AAU)

Chuo Kikuu cha Uongozi cha Afrika (ALU)
Chuo Kikuu cha Uongozi cha Afrika (ALU)

Chuo Kikuu cha Uongozi cha Afrika (ALU) ni taasisi kuu duniani ya elimu ya juu iliyo na mabewa nchini Rwanda na Morisi. Wanafunzi wa ALU wamekuwa wachangiaji amilifu katika miradi mbalimbali ya ESSA. ESSA pia imehamasisha kazi ambayo ALU na INSEAD wanafanya sasa katika elimu ya utendaji. 

Chuo Kikuu cha Uongozi cha Afrika (ALU) 

Agence Française de Developpement (AFD)
Agence Française de Developpement (AFD)

Agence Française de Developpement ni benki ya maendeleo ya umma ya Ufaransa. Inatoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa miradi katika nchi zinazoendelea na zinazochipuka. Idara ya Utafiti ya AFD imeshirikiana na ESSA na NORRAG ili kusaidia utafiti kuhusu elimu Afrika Magharibi ya Frankofoni, hasa Bukina Faso. Kwa pamoja, tumefadhili AREB (Atelier de Recherche sur l'Education au Burkina Faso) mjini Ouagadougou, Bukina Faso, huku kongamano lao "L’éducation au Burkina Faso: progrès, défis actuels et perspectives" likiwa mwezi Novemba 2017.

"ESSA ni mshirika mpya mzuri katika sekta ya elimu na ninafurahia sana wanafanya kazi pia katika Afrika ya Frankofoni na wanaunga mkono sana utafiti wa Kiafrika kuhusu elimu. Kuna haja ya kuunganisha Frankofoni na Anglofoni, na ESSA inaweza kuongeza thamani kubwa hapa".

Rohen D'Aiglepierre, Mwanauchumi wa Maendeleo ya Binadamu, Afisa wa Utafiti, Idara ya Utafiti ya Agence Française de Développement (AFD).

 

Agence Française de Developpement (AFD)

Ashesi
Ashesi

Ashesi is increasingly recognized as one of the finest universities in Africa, with an educational experience proven to prepare students for successful lives and careers. Their mission is to educate ethical, entrepreneurial leaders in Africa;

to cultivate within students, the critical thinking skills, the concern for others, and the courage it will take to transform the continent.  With an academic program designed in collaboration with some of the world's best universities and organisations, Ashesi has created an educational model unlike any other in Africa.

Ashesi has partnered with ESSA through ESSA’s paid internships for African students, giving them the opportunity to fully take part in a number of educational projects.

Ashesi

Atelier de Recherche sur l’Education au Burkina Faso (AREB)
Atelier de Recherche sur l’Education au Burkina Faso (AREB)

Atelier de Recherche sur l’Education au Burkina Faso (AREB)  ni Mradi ya kujiunga na watafiti wa elimu wa Bukinafaso na kutoa fursa za mazungumzo pamoja na watunga sera nchini humo. ESSA imefurahia kusaidia kazi ya AREB kwa kuunga mkono kongamano lao "L’éducation au Burkina Faso: progrès, défis actuels et perspectives" la mwezi Novemba 2017

Atelier de Recherche sur l’Education au Burkina Faso (AREB)

Dubai Cares
Dubai Cares

Since its inception, Dubai Cares, part of Mohammed bin Rashid Al Maktoum Global Initiatives, has been working towards providing children and young people in developing countries with access to quality education. As a result, the UAE-based global philanthropic organization has successfully launched education programs reaching over 18 million beneficiaries in 57 developing countries.

Dubai Cares support programs in early childhood development, access to quality education, technical and vocational education and training for youth as well as a particular focus on education in emergencies.

“We are excited to announce our expansion into tertiary education, in partnership with ESSA. We believe this will help connect millions of students and graduates to employment opportunities and will be central to developing successful and sustainable economies and societies."

Dr. Tariq Al Gurg, Chief Executive Officer at Dubai Cares

Dubai Cares

ESMT (European School of Management and Technology)
ESMT (European School of Management and Technology)

Shule ya kimataifa ya biashara ya nchini Berlin ilianzishwa na makampuni na taasisi 25 za kimataifa zinazoongoza. Inatoa mipango mbalimbali ya shahada za uzamili pamoja na elimu ya utendaji inayoangazia uongozi, wajibu wa jamii, ushindani wa Ulaya na usimamizi wa teknolojia.  

ESMT inafanya kazi na ESSA kwenye kazi yake ili kuunda msururu wa programu na rasilimali za kutengeneza viongozi wa elimu.

ESMT (European School of Management and Technology)

Serikali ya Ghana, Baraza la Kitaifa la Elimu ya Juu (NCTE)
Serikali ya Ghana, Baraza la Kitaifa la Elimu ya Juu (NCTE)

Baraza la Kitaifa la Elimu ya Juu (NCTE) la Ghana lilianzishwa mwaka 1993 kama shirika simamizi la Elimu ya Juu nchini Ghana.  NCTE imejitolea kutoa uongozi katika mwelekeo, kazi, jukumu na umuhimu wa elimu ya juu nchini Ghana, na kuongoza Elimu ya Juu hadi ngazi mpya.

Baraza la Kitaifa la Elimu ya Juu (NCTE) la Ghana

Hasso Plattner Institut (HPI)
Hasso Plattner Institut (HPI)

Taasisi ya Hasso-Plattner (HPI) iliyoko Potsdam iliundwa na Prof. Hasso Plattner, mwanzilishi mwenza wa SAP. HPI ni mojawapo ya vitui vikuu vya elimu kote duniani katika nyanja ya mafunzo ya kidijitali na kozi na rasilimali zake za mafunzo zilizo wazi zinawawezesha watu wa umri wote kote ulimwenguni kuongeza ujusi wao wa kidijitali.

HPI ni mshirika wa kiteknolojia wa ESSA katika kuendeleza dhana ya Kituo cha Maarifa cha 'kutegemewa'  kwa kila kitu kinachohusiana na 'Elimu katika Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara'. Zaidi ya hayo, HPI imetoa kwa ESSA jukwaa la OpenESSA ambalo tutatumia kwa rasilimali mbalimbali za mtandaoni kutoka kwa wachangiaji wadogo hadi kwa MOOCs.  Tutazalisha hizi kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya Afrika na washirika wengine. 

Ushirikiano na ESSA ni fursa kwa HPI ya kuwa ya Kiafrika zaidi. Tunafurahia mtazamo wa kuona OpenESSA ikizinduliwa mwishoni mwa mwaka, kwa ushirikiano nasi, na kufikia watumiaji wengi zaidi Waafrika wa maudhui ya ubora wa juu ya kujifunza kidijitali mtandaoni".

Prof. Christoph Meinel, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji, Hasso Plattner Institute for Digital Engineering gGmbH 

Hasso-Plattner Institute (HPI)

Logo: INSEAD
INSEAD

INSEAD ni moja ya shule za biashara zinazoongoza duniani na ESSA iliunda ushirikiano na INSEAD mwezi Machi 2017.

 Hatua ya kwanza ya ushirikiano baina ESSA na INSEAD imekuwa kuwaunganisha na Chuo Kikuu cha Uongozi cha Afrika (ALU), ikizingatia msururu wa miradi ya ramani, na kutengeneza mipango ya viongozi katika elimu.  

INSEAD
 

Inter University Council for East Africa (IUCEA)
Inter University Council for East Africa (IUCEA)

The Inter University Council for East Africa (IUCEA) was established in 1980, originally called the Inter University Committee (IUC).  IUCEA is hosted in Kampala, Uganda with its main objectives being to:

  • Facilitate networking among universities in East Africa, and with universities outside the region;

  • Provide a forum for discussion on a wide range of academic and other matters relating to higher education in East Africa; and

  • Facilitate maintenance of internationally comparable education standards in East Africa so as to promote the region's competitiveness in higher education.

With its main roles and functions to:

  • Coordinate inter-university cooperation in East Africa;

  • Facilitate the strategic development of member universities; and

  • Promote internationally comparable higher education standards and systems for sustainable regional development.

IUCEA and ESSA's first cooperation will be the Scholarship Impact Hub.

IUCEA

Logo: Wakfu wa Jacobs
Wakfu wa Jacobs

Wakfu wa Jacobs, una lengo kuu la kukuza maendeleo ya watoto na vijana kote duniani, na kutoa aina mbalimbali za msaada kwa watu binafsi na taasisi zinazofanya kazi katika utafiti na mazoea. Nchini Kodivaa, wanafanya kazi ili kusaidia kubadilisha elimu, katika ngazi ya kitaifa na mashambani.

Kuona thamani ya ushirikiano baina ya ESSA na Kituo cha REAL katika Chuo Kikuu cha Cambridge ili kubadilisha uonekanaji na upatikanaji wa utafiti kuhusu elimu uliyofanywa na watafiti walio Afrika, Wakfu wa Jacobs sasa ni mfadhili muhimu wa kazi hii. Wakfu wa Jacobs pia unasaidia ESSA katika mradi nchini Kodivaa wa kufanya utafiti kuhusu elimu na mafunzo na vilevile utafiti kuhusu uhusiano kati ya vikoa viwili na uwezekanaji wa kuwaajiri vijana. Kama wakfu muhimu katika sekta ya elimu, Wakfu wa Jacobs pia umesaidia sana ESSA katika kujenga wasifu na uhusiano wake barani Afrika Magharibi.

Wakfu wa Jacobs

Chuo Kikuu cha Jacobs
Chuo Kikuu cha Jacobs

Chuo Kikuu cha Jacobs ni chuo kikuu cha lugha ya Kiingereza, kinachotoa viwango vya juu zaidi katika utafiti na mafundisho, kilichoko mjini Bremen, Ujerumani. Ina wanachama wengi ambao ni wanafunzi Waafrika kutoka nchi na asili mbalimbali.

Chuo Kikuu cha Jacobs kimeshirikiana na ESSA kwa njia kadhaa ikijumuisha warsha pamoja na wanafunzi wake Waafrika, miradi iliyolipwa ili kusaidia shughuli zetu za mitandao ya kijamii.

"Tumekuwa tukifanya kazi pamoja na ESSA kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, hasa katika miradi ya wanafunzi, na kuwaruhusu wanafunzi Waafrika kutoka Chuo Kikuu cha Jacobs kuwa sehemu ya kazi nzuri ya ESSA kuhusu elimu. Tunathamini sana kwamba ESSA inawaweka vijana Waafrika katika kitovu cha yote wanayofanya."

 Tanja Woebs, Afisa wa Uhusiano wa Kampuni na Mipango ya Talanta, Suluhu za Biashara, Chuo Kikuu cha Jacobs

Chuo Kikuu cha Jacobs  

Logo: Mastercard Foundation
Wakfu wa MasterCard

WAKFU WA MASTERCARD  ni mojawapo ya wakfu zinazoongoza ulimwenguni katika nyanja ya elimu ya juu, na una uwepo mkubwa barani Afrika hasa katika kujenga uwezo na ufadhili wa kimasomo.  WAKFU WA MASTERCARD ni mshirika wa kawaida wa ESSA kwenye mradi wa "Demografia za Kitivo" na kwa shauku umetoa fedha kwa ajili ya majaribio ya Ghana na vilevile msaada na michango mingine.

Wakfu wa MasterCard 

Logo: NORRAG
Mtandao wa sera na ushirikiano wa kimataifa katika elimu na mafunzo (NORRAG)

Mtandao wa sera na ushirikiano wa kimataifa katika elimu na mafunzo (NORRAG) jukumu lake kuu ni kuzalisha, kusambaza na kutoa maarifa muhimu na kujenga uwezo kwa ajili ya na pamoja na wadau mbalimbali. Wadau hawa wanatengeneza na kubuni sera na mazoea ya elimu, katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

NORRAG na ESSA wameungana na AFD ili kusaidia utafiti kuhusu elimu barabi Afrika Magharibi ya Frankofoni, hasa Bukina Faso. Mkurugenzi wa ESSA pia amezungumza katika kikao cha kimataifa cha NORRAG kuhusu "Utoaji Misaada katika Elimu: Mitingo ya Ulimwengu, Tofauti za Kikanda na Mitazamo Tofauti" mwezi Novemba 2017, mjini Geneva, Uswisi.  

Mtandao wa sera na ushirikiano wa kimataifa katika elimu na mafunzo (NORRAG)

Logo: Ofisi ya Idadi ya Watu (PRB)
Ofisi ya Idadi ya Watu (PRB)

Ofisi ya Idadi ya Watu (PRB), mjini Washington DC, ni mojawapo ya taasisi za kidemografia zinazoongoza duniani. Inawafahamisha watu kote duniani kuhusu idadi ya watu, afya, na mazingira, na kuwawezesha kutumia taarifa hiyo ili kuendeleza ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo. Bidhaa yake kuu ni Karatasi ya Takwimu za Idadi ya Watu Duniani.

PRB hufanya kazi na AAU pamoja na ESSA kwenye mradi wa Demografia ya Kitivo 

"ESSA ina malengo makubwa ya kukabiliana na vikwazo vya utaratibu katika kuongeza faida katika uwekezaji unaofanywa kwenye elimu ya juu katika nchi za Afrika."

Jeff Jordan, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji

Ofisi ya Idadi ya Watu (PRB)

Robert Bosch Stiftung
Robert Bosch Stiftung

Robert Bosch Stiftung ni wakfu wa kibinafsi wa Ulaya na mfadhili mkuu wa ESSA ilipokuwa inaazishwa.

Wakfu wa Bosch pia umetoa msaada mkubwa usio wa kifedha pamoja na kumuunga mkono mkurugenzi mwanzilishi wa ESSA, Olaf Hahn, kutoa msaada wa bodi kwa njia ya udhamini wa Afisa Mkuu Mtendaji wao, Uta-Micaela Dürig na vilevile ufikiaji mtandao wake mkubwa wa mahusiano barani Afrika na kote ulimwenguni.

“ESSA has developed tremendously over the last three years. The seed-funding provided by us is offering high return on investment. I am excited to see ESSA growing further, and to produce high impact for Tertiary Education in sub-Saharan Africa.”

Joachim Rogall, President and CEO, Robert Bosch Stiftung

Robert Bosch Stiftung

The Regional Universities Forum for Capacity Building in Agriculture (RUFORUM)
The Regional Universities Forum for Capacity Building in Agriculture (RUFORUM)

The Regional Universities Forum for Capacity Building in Agriculture (RUFORUM), established by ten Vice Chancellors in 2004, is a consortium of 121 African universities operating within 38 countries spanning the African continent.

RUFORUM is coordinated by a Secretariat hosted by Makerere University in Kampala, Uganda. The consortium will be a key partner for ESSA in the next phase of our strategy. 

The Regional Universities Forum for Capacity Building in Agriculture (RUFORUM).

SAP
SAP

SAP ni kiongozi wa soko katika programu ya kutumiwa katika biashara na husaidia mashirika kupambana na athari za uharibifu wa utata, kuzalisha fursa mpya za ubunifu na ukuaji na kukaa kifua mbele katika ushindani.  

SAP imesaidia ESSA kubuni mradi wao wa "Kituo cha kutegemewa cha Maarifa kuhusu elimu barani Afrika", katika mfumo wa "likizo ya kijamii" inayoruhusu timu za SAP kufanya kazi na mashirika yasiyo ya serikali na ya misaada kuhusu masuala ya kidijitali. 

SAP
 

The Schaufler Foundation
The Schaufler Foundation

The Schaufler Foundation was founded in 2005 by Senator h. c. Peter Schaufler (deceased), former CEO and owner of BITZER, with the aim to continue his life’s work of combining entrepreneurship with science, research, education and the arts.

In terms of science and research, the focus is on environment protection. In the field of education, the foundation supports a variety of universities in Germany and now, by working with ESSA, will expand its activities into Africa.  The Schaufler Foundation is a key funder of ESSA's Pilot Scholarship Impact Hub project.

The Schaufler Foundation also funds the Schauwerk Sindelfingen, a museum for contemporary art.  Since its opening in June 2010, the Schauwerk Sindelfingen has displayed a representative selection of over 3,500 works from the Schaufler collection, together with loans from other museums and collectors as part of its temporary exhibitions.

The Schaufler Foundation

 

Logo: Chuo Kikuu cha Cambridge
Chuo Kikuu cha Cambridge

Kituo cha Utafiti wa Ufikiaji Sawa na Mafunzo (Kituo cha REAL) ni mojawapo ya taasisi kuu ulimwenguni za utafiti kuhusu elimu, kilichoko katika mojawapo ya vyuo vikuu vikuu zaidi duniani. Misheni ya Chuo Kikuu cha Cambridge ni kuchangia kwa jamii kwa njia ya kutafuta elimu, kujifunza na utafiti katika ngazi za juu zaidi kimataifa za ubora. Vipaumbele vya Kituo cha REAL vinaambatana na, na kuchangia kwenye, mkakati wa kimataifa wa Chuo Kikuu hiki.

Kitivo cha Elimu ni muhimu kwa misheni ya Chuo Kikuu na kila wakati kinapata matokeo bora. Matokeo ya mafundisho na utafiti wake thabiti ni athari kubwa ulimwenguni na wasomi wake wanashauri serikali mbalimbali kote duniani kuhusu sera na miradi yake ya ushirikiano ya kimataifa inayoathiri mabadiliko mashinani.

Kituo cha REAL kinatumia rekodi hii nzuri, na kuunganisha na kuimarisha uwezo wa Kitivo na kuunda utaalamu umuhimu katika elimu na maendeleo ya kimataifa ili kuendeleza ajenda yake. Inajenga juu ya kazi muhimu iliyofanyika hapo awali chini ya Kituo cha Elimu ya Jumuiya ya Madola na Kituo cha Elimu na Maendeleo ya Kimataifa (CEID), hasa mpango wa RECOUP.

Kituo cha Utafiti wa Ufikiaji Sawa na Mafunzo (Kituo cha REAL)

Chuo Kikuu cha Warwick
Chuo Kikuu cha Warwick

Chuo Kikuu cha Warwick kimekuwa mshirika muhimu kwa ESSA, hata kabla haijaanzishwa.  Kichocheo cha kuunda ESSA kilikuwa uzoefu wa mwanzilishi wake aliyekuwa mwanafunzi wa zamani wa Warwick, Patrick Dunne, katika kuanzisha na kukuza msaada mwingine pamoja na Warwick, Warwick barani Afrika (WIA).  Tangu mwaka wa 2006 WIA imewafaidi zaidi ya vijana 465,000 Waafrika katika maeneo yaliyopunguzwa na ya mashinani kwa mafundisho ya Hisabati na Kiingereza.  Warwick pia ilitoa msaada na hamasisho katika ushahidi wa kwanza wa utafiti wa dhana ya ESSA.

Tangu kuanzishwa kwa ESSA, Warwick imehusika moja kwa moja katika miradi mitatu muhimu:

  • Kama sehemu ya mbinu ya ESSA ya kuweka Waafrika kwenye kitovu cha yote ifanyayo, wanafunzi na walimu katika Warwick barani Afrika (link) wameshiriki katika msururu wa warsha kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili nchini Tanzania na Afrika Kusini. Warsha hizi hazijaimarisha mkakati na vipaumbele vya ESSA tu bali pia zimeongeza sauti imara ya Afrika.   

  • Mradi wa Hali ya Takwimu wa ESSA unafaidika sana kutokana na jukumu la ushauri ambao Profesa Jane Hutton ni kucheza na hatimaye;

  • Tovuti ya kazi za kitaaluma ya Warwick Jobs.ac inashirikiana na Chama cha Vyuo Vikuu Afrika na ESSA ili kuunda bodi ya kazi ya kitaaluma za mtandaoni za Pan-Afrika.

Chuo Kikuu cha Warwick

Warwick barani Afrika