Kubadili uonekanaji na upatikanaji wa utafiti wa Kiafrika Afrika ya Jangwa la Sahara

Kubadili uonekanaji na upatikanaji wa utafiti wa Kiafrika Afrika ya Jangwa la Sahara

Kubadili uonekanaji na upatikanaji wa utafiti wa Kiafrika Afrika ya Jangwa la Sahara

Mojawapo ya sababu za kutengeneza ESSA ilikuwa mfadhaiko wa Mwanzilishi kujaribu kutafuta utafiti muhimu unaohusiana na kubadilisha elimu barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.

Huku wengi wakijitahidi ili kuboresha hali hii na kuna ushahidi mkubwa wa kuhamasisha sera na mazoea, tathmini ya kiutaratibu ya utafiti uliofanywa ndani ya Afrika ya Jangwa la Sahara ili kutambua matatizo na suluhu haupatikani. 

 

ESSA na Kituo cha REAL katika Chuo Kikuu cha Cambridge vimejenga ushirikiano ili kujaza pengo hili kwa kutoa ramani ya utafiti wa umuhimu wa kufanikisha SDGs zilizofanywa na watafiti wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara katika taasisi za Kiafrika.

Ushirikiano wa sasa unatafuta

  • Kuweka ramani ya utafiti wa elimu kulingana na ushahidi uliofanywa na watafiti wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, taasisi na mitandao ili kuzalisha fasihi: hifadhidata inayopatikana wazi na tangamanifu inayoweza kutafutwa kulingana na mada, nchi na taasisi.

  • Tathmini na upitie fasihi ili kutambua mandhari ya kawaida, matokeo makuu, na mapengo ya utafiti, na hivyo

  • Toa mwelekeo wa sera na mazoea yenye msingi wa ushahidi na utambue vipaumbele na ushirikiano wa utafiti wa baadaye.

Katika kufanikisha malengo haya, kuna mashauriano na watafiti kote barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara na kwingineko. Hii itahakikisha matumizi ya matokeo ya mradi na urithi wake baada ya mradi kukamilika na kuweka misingi kwa ajili ya ushirikiano wa baadaye wa utafiti

Kituo cha REAL na ESSA vitafanya matokeo ya mapema ya mchakato wa ramani yanayopatikana kwa lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa huku Kireno kikipatikana hivi karibuni. ESSA imetoa fedha kama mbegu kwa ajili ya mradi huu. Kwa kushirikiana na Wakfu wa Jacobs  tunaendelea kuunga mkono kazi hii hadi katika awamu inayofuata. 

Malengo Yetu

 

Washirika wetu katika Kubadili uonekanaji na upatikanaji wa utafiti wa Kiafrika barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara

Logo: Chuo Kikuu cha Cambridge
Chuo Kikuu cha Cambridge

Kituo cha Utafiti wa Ufikiaji Sawa na Mafunzo (Kituo cha REAL) ni mojawapo ya taasisi kuu ulimwenguni za utafiti kuhusu elimu, kilichoko katika mojawapo ya vyuo vikuu vikuu zaidi duniani. Misheni ya Chuo Kikuu cha Cambridge ni kuchangia kwa jamii kwa njia ya kutafuta elimu, kujifunza na utafiti katika ngazi za juu zaidi kimataifa za ubora. Vipaumbele vya Kituo cha REAL vinaambatana na, na kuchangia kwenye, mkakati wa kimataifa wa Chuo Kikuu hiki.

Kitivo cha Elimu ni muhimu kwa misheni ya Chuo Kikuu na kila wakati kinapata matokeo bora. Matokeo ya mafundisho na utafiti wake thabiti ni athari kubwa ulimwenguni na wasomi wake wanashauri serikali mbalimbali kote duniani kuhusu sera na miradi yake ya ushirikiano ya kimataifa inayoathiri mabadiliko mashinani.

Kituo cha REAL kinatumia rekodi hii nzuri, na kuunganisha na kuimarisha uwezo wa Kitivo na kuunda utaalamu umuhimu katika elimu na maendeleo ya kimataifa ili kuendeleza ajenda yake. Inajenga juu ya kazi muhimu iliyofanyika hapo awali chini ya Kituo cha Elimu ya Jumuiya ya Madola na Kituo cha Elimu na Maendeleo ya Kimataifa (CEID), hasa mpango wa RECOUP.

Kituo cha Utafiti wa Ufikiaji Sawa na Mafunzo (Kituo cha REAL)

Logo: Wakfu wa Jacobs
Wakfu wa Jacobs

Wakfu wa Jacobs, una lengo kuu la kukuza maendeleo ya watoto na vijana kote duniani, na kutoa aina mbalimbali za msaada kwa watu binafsi na taasisi zinazofanya kazi katika utafiti na mazoea. Nchini Kodivaa, wanafanya kazi ili kusaidia kubadilisha elimu, katika ngazi ya kitaifa na mashambani.

Kuona thamani ya ushirikiano baina ya ESSA na Kituo cha REAL katika Chuo Kikuu cha Cambridge ili kubadilisha uonekanaji na upatikanaji wa utafiti kuhusu elimu uliyofanywa na watafiti walio Afrika, Wakfu wa Jacobs sasa ni mfadhili muhimu wa kazi hii. Wakfu wa Jacobs pia unasaidia ESSA katika mradi nchini Kodivaa wa kufanya utafiti kuhusu elimu na mafunzo na vilevile utafiti kuhusu uhusiano kati ya vikoa viwili na uwezekanaji wa kuwaajiri vijana. Kama wakfu muhimu katika sekta ya elimu, Wakfu wa Jacobs pia umesaidia sana ESSA katika kujenga wasifu na uhusiano wake barani Afrika Magharibi.

Wakfu wa Jacobs