12 Mar, 2018

Hadithi yetu hadi sasa

ESSA imekua kwa haraka tangu tulipoanzishwa rasmi mwaka wa 2016.

Je, mawazo yakutengeneza ESSA yalitoka wapi?

Mawazo yaliyopelekea kutengenezwa kwetu yalikuwa ni tokeo la mchanganyiko mzuri wa hisia za mfadhaiko na kuona fursa.  Mfadhaiko ulitokana na uzoefu wa mwanzilishi wetu wa kusaidia kujenga [Warwick in Africa] [link], shirika la msaada lenye mafanikio makubwa la kuwafundisha watoto na kuwafunza walimu katika makazi duni na katika maeneo ya mashambani yaliyo na umaskini mkubwa. 

Fursa alizoziona, zilitoka mahali sawia na pale alipoona njia za kufanya kazi na wengine ili kusaidia kutatua baadhi ya masuala magumu zaidi ya kimfumo, na kuwahamasisha watu wengi ambao walijua nini kinachohitajika kufanywa lakini hawakuwa na rasilimali au uhusiano wa kubadilisha mambo na wale waliokuwa nao. 

Uhakika wake mkubwa ni kwamba Waafrika wanapaswa kuwa kitovu cha kila kitu ambacho ESSA ingefanya. Hii ilianza na msururu wa warsha za wanafunzi na walimu katika shule kote katika kanda ili kuwafahamisha kile ambacho ESSA inaweza kufanya.


Dhana ya kwanza rasmi ya ESSA ilikuwa ni kuzingatia mambo manne:

 • "Kujiunga" 

 • Kuunda kituo cha Maarifa cha “Kutegemewa”

 • Kusaidia kujenga uwezo na;

 • Kusaidia kujenga uwezo na;

Kama unaweza kuona, miaka miwili tu tangu kutengenezwa, mawazo haya ya kwanza sasa yanakuwa uhalisia. Waafrika kwa kweli wamo katika kitovu cha kufanya mambo kutendeka katika ESSA na ESSA inaanza kufanya tofauti.


ESSA ilianzaje?

Kumekuwa na awamu tatu wazi hadi sasa:

"Msaada wa mbegu na kuthibitisha mfano"

"Kuchangisha mitaji muhimu ya kuanza kutoka Wakfu wa Bosch" na kisha

"Kuunda ushirikiano [link Our partners], kukuza fedha za mradi na kuendelea na kazi (link) ili kuthibitisha thamani ambayo ESSA inaweza kuleta".

Mbali na kutoa uwekezaji mkubwa, Wakfu wa Bosch pia ulitoa msaada wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na, kwa kiasi kikubwa, uungwaji mkono wa Olaf Hahn kama Mkurugenzi Mwazilishi wetu

 Pamoja na seti ya principles kuongoza kazi yetu imeendesha maendeleo yetu na kutusaidia kujenga uwezo na mahusiano muhimu ili kuanza kuanzisha ESSA kwa muda mrefu.

Kama unavyoona kutokana na Our work  miradi yetu ya kwanza na ushirikiano tumejenga kasi kubwa na wakati mwingine, kama vile kazi yetu kuhusu demografia za kitivo na kuhusu kubadilisha uonekanaji na upatikanaji wa utafiti uliofanywa na watafiti Waafrika, tayari imeanza kuibua hamasisho na kubadili majadiliano. 

Tuna kazi nyingi ya kufanya na tunatambua kuwa, kama vijana wengi Waafrika tunajaribu kusaidia, tuko mbali kutimiza uwezo wetu. Tunatarajia utahamasishwa na kile tunachotenda, ungependa get involved na utusaidie kuwasaidia na watimiza haya kwa haraka zaidi.


Kwa nini msisitizo wa kwanza umehusu Elimu ya juu?

Moja ya principles muhimu zaidi imekuwa kuwa na "Mtazamo wa hatua kwa hatua". Tunajitahidi kuchangia kufanya kazi katika nyanja nzima ya elimu katika maeneo mengi katika nchi zilizo na sifa na tamaduni nyingi tofauti. Tulihitaji kuanza mahali fulani na kuepuka kujaribu kujisambaza katika maeneo machache.  

Elimu ya juu ni mahali pa kuanzia. Taasisi za elimu ya juu ni vipengele muhimu vya elimu katika kanda, kwa kawaida zinawafundisha walimu, ni karibu na soko la ajira, zinafanya utafiti kuhusu elimu na zinashawishi sera ya kitaifa na kikanda. Pia ni njia ya asilia kuelekea sehemu nyingine za sekta hii.


Kwa hivyo ni kipi kinafuata?

Vipaumbele vyetu vya sasa ni:

 • Kuwasilisha athari kubwa kutokana na kazi yetu ya sasa.

 •  Kujenga na kuwasilisha jukwaa letu la rasilimali la dijitali na mshirika wetu Hasso Plattner Institute.

 • Kuanzisha rasmi jopo la vijana wetu wa pan-Afrika na Mwenyekiti wake kujiunga na bodi ya wadhamini ya ESSA. 

 •  Kukamilisha kazi na kuchangisha pesa ili kupeleka kituo chetu cha Maarifa ambacho ni kichanga hadi hatua inayofuata.

 • Kazi yetu kuhusu hali ya data ya kielimu na uwezo wa sayansi ya data katika kanda kuanzia uzinduzi hadi hatua ya majaribio. 

 • Pamoja na washirika wetu, kuanzisha mipango yetu ya kwanza ya maendeleo kwa viongozi wa elimu. 

Comments

About text formats

Restricted HTML

 • Allowed HTML tags: <a href hreflang> <em> <strong> <cite> <blockquote cite> <code> <ul type> <ol start type> <li> <dl> <dt> <dd> <h2 id> <h3 id> <h4 id> <h5 id> <h6 id>
 • Lines and paragraphs break automatically.
 • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.